December 28, 2019



UONGOZI wa KMC umesema kuwa kwa sasa akili zao ni kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba utakaochezwa leo Desemba 28 uwanja wa Uhuru.

KMC ipo nafasi ya 17 imekuwa na msimu wa kusuasua kutokana na kushindwa kufurukuta kwenye mechi 12 walizocheza ina pointi 9 ikiwa ilishinda mechi mbili pekee sare tatu na kichapo saba.

Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa wanatambua kwamba hawajawa na msimu mzuri ila watapambana kurejea kwenye ubora wao.

“Kila kitu ni hatua kwani hakuna mchezaji anayependa kupata matokeo mabovu ila kutokana na ushindani na kipindi cha mpito tunakutana na haya ila hatutapenda kuziacha pointi tatu mbele ya Simba ni muhimu kwetu na tunapambana, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

2 COMMENTS:

  1. pole yenu coz simba nasi tunahitaji point zenu ety

    ReplyDelete
  2. Hapana panic kwasababu mtazipata na Kocha Mkwasa keshasema kuwa Simba ni timu ya kawaida tu kwaahivo timu hizo mbili kila moja kwaurahisi mutapata point tatu tatu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic