December 23, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umesema baada ya kumalizana na mabeki wawili Lamine Moro na Andrew Vincent 'Dante' umedai kwa sasa hakuna ulazima wa kutumia gharama zaidi ya milioni 80 kumsajili beki wa Klabu ya Coastal Union Bakari Nondo Mwamnyeto.

Taarifa zinasema Yanga inaona Lamine Moro na Dante wakiongozwa na Kelvin Yondani wataiongoza safu hiyo ya ulinzi kwa sahihi zaidi.

Yanga ilikuwa inapigania kwa udi na uvumba saini ya mchezaji huyo ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Stars kilichocheza mashindano ya CECAFA nchini Uganda.

Kwa sasa uongozi wa Yanga umesema utaendelea kuboresha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wengine ambao itaendelea kuwatangaza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic