Ofisa Habari wa KMC FC, Anuary Mbinde, amewataka mashabiki na wanachama wa Simba kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Uhuru leo ili kuwapa hamasa.
KMC itakuwa na na kibarua kizito dhidi ya Yanga katika mechi ambayo itapigwa majira ya saa 10 kamili za jioni.
Ofisa huyo anaamini wanaweza kufanya vema katika mechi huyo na akiichukulia Yanga kama timu zingine ambazo zinashiriki ligi.
Ameeleza wameshajiandaa licha ya kuwa na matokeo mabaya katika mechi za hivi karibuni lakini kwa leo watakuwa tayari kupata matokeo.
"Tunawaoomba wapenzi na mashabiki wa Simba waje kutupa sapoti leo.
"Tunaamini watakuwa na msaada juu ya uwepo wao na tutaweza kufanya vema vizuri.
"Sisi tupo tayari kwa ajili ya mechi na naimani tutafanya vema."
0 COMMENTS:
Post a Comment