December 17, 2019


Inaelezwa uongozi wa Klabu ya Simba kupitia Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingiza raia wa Afrika Kusini umemtimua kazi aliyekuwa meneja wa mradi wa Uwanja wa Simba Mo Arena, Richard Robert kutokana na madai ya usimamizi mbovu wa miundombinu ya ujenzi kwenye uwanja huo.

Mazingiza amefikia hatua ya kumuondoa meneja huyo ambaye alikuwa anasimamia ujenzi huo kufuatia madai ya kutoridhishwa na ubora wa uwanja wa nyasi asilia aliokuwa akiusimamia.

Taarifa uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinasema kuwa kiongozi huyo ameondolewa baada ya mtendaji mkuu kufanya ukaguzi wakati ujenzi ulipokuwa ukiendelea kufuatia kuona upungufu.

“Meneja amesimamishwa kazi kwa muda sasa na mtendaji mkuu kutokana madai ya kushindwa kusimamia, vyema miundombinu ya uwanja hasa wa nyasi asilia ndiyo maana haonekani kwa sasa,” kilisema chanzo.

Championi lilimtafuta Mazingiza kwa njia ya simu lakini simu yake haikupokelewa kwa ajili ya kuelezea suala hilo.

Ikumbukwe Robert huyo awali alikuwa meneja katika upande wa timu lakini alifungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ kwa madai ya kuihujumu Taifa Stars kabla ya kufunguliwa na kupewa majukumu ya kusimamia Uwanja Simba Mo Arena ambao umeanza kutumika.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic