December 4, 2019


KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa ‘Master’ amekiri kikosi chake kuwa na upungufu huku akiahidi kukifanyia maboresho kwa kusajili wachezaji wenye hadhi na uwezo wa kuichezea timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara na KMC uliochezwa juzi Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Yanga imepanga kuifanyia maboresho safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na David Molinga ‘Falcao’, Juma Balinya, Maybin Kalengo, Issa Bigirimana na Sadney Urikhob.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkwasa alisema kuwa hakuna ubishi kikosi chao kinahitaji maboresho makubwa, kati ya hayo ni lazima waifumue safu ya ushambuliaji kwa kuleta wengine wapya wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao.


Mkwasa alisema kuwa timu yake imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi lakini umaliziaji ni tatizo, hivyo ni lazima wasajiliwe washambuliaji wengine wenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao huku straika rasta wa Biashara United, Mnigeria Innocent Edwin aliyewahi kuwafunga Simba msimu uliopita akikaribia kukamilisha usajili wake Jangwani.

“Lipo wazi kabisa ni lazima Yanga tufanye usajili katika dirisha utakaoendana na timu yetu na kikubwa tunataka kuona tunafanya marekebisho kwenye kila sehemu itakayokuwa na upungufu ikiwemo hiyo ya ushambuliaji ambayo ndiyo yenye matatizo.

“Hilo limeonekana katika michezo ya ligi iliyopita timu imetengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umaliziaji ni tatizo kutokana na umakini mdogo wa washambuliaji tulionao katika timu,” alisema Mkwasa.

5 COMMENTS:

  1. Yanga bado wana mambo ya kizamani sana ya kusajili mchezaji eti kwa sababu aliifunga Simba. Kwenye ligi inayoendelea amefunga magoli mangapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tutajie mchezaji ambaye alisajiriwa yanga lwa kigezo cha kuifunga simba...hizi blogs mnaziamini sana

      Delete
  2. Katika wachezaji bomu Molinga ni mmojawapo. Afadhali huyo wa Biashara.

    ReplyDelete
  3. namuona Molinga kama fowadi mzuri ambaye anakosa mlishaji ......shida ni kwamba lazima timu ixhezd mfumo wa kuendana na Molinga yaani 4-4-2

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic