December 25, 2019


BENO Kakolanya, nyota wa Simba ameweka rekodi yake mpya ndani ya Bongo kwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara akiwa na Simba.

Kakolanya ambaye alisajiliwa na Simba akitokea Yanga hakucheza mchezo wowote wa ligi kati ya ile 10 ambayo Simba ilicheza.

Kwenye mechi zote 10 langoni alikaa mlinda mlango namba moja Aishi Manula ambaye leo alianza benchi.

Manula alifungwa mabao matatu pekee kwenye mechi hizo 10 ambapo hajafungwa bao hata moja la penalti ila amefungwa bao moja la nje ya 18 mbele ya JKT Tanzania na mawili ya ndani ya 18 dhidi ya Mwadui FC na Mtibwa Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic