December 25, 2019


Inaelezwa kuwa straika wa UD Songo ya Msumbiji, Luís Miquissone, tayari ameshamalizana kila kitu na Simba Sports Club.

Taarifa zinasema tayari mabosi wa Simba wamemalizana naye na inawezekana akatambulishwa muda wowote kuanzia sasa.

Luis anakumbukwa kwa bao lake ambalo aliwafunga Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika jijini Dar es Salaam, mechi ambayo ilimalizika kwa sare ya 1-1.

Inaelezwa kuwa Luis atakuwa mbadala wa Emmanuel Okwi ambaye tangu aondoke mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara walikuwa hawajasajili mbadala wake.

4 COMMENTS:

  1. Kimya Kimya bila ya makelele. Mmoja au Wawili wanatosha kwani wapishi wakiwa wengi chakula chaharibika ndio siasa ya Mnyama mkali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic