December 13, 2019





Na Saleh Ally
SHIRIKISHO la Soka Zambia (FAZ), liliamua kutoongeza
mkataba mpya kwa kocha Sven Vandenbroeck raia wa
Ubelgiji kundelea kuinoa Chipolopolo baada ya kuona
alishindwa kufanya kile walichokihitaji.


FAZ iliingia mkataba mfupi na Vandenbroeck na sharti
namba moja ni kuhakikisha Chipolopolo inafuzu kucheza
katika Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019) lakini akafeli.
Vandenbroeck alifeli baada ya kuingoza Zambia
kushinda mechi moja, sare moja na kupoteza moja. FAZ
wakaona hakukuwa na sababu ya kumuongezea
mkataba tena kutokana uhalisia.


Machi 23, safari yake ndani ya Chipolopolo ikaishia hapo
na nafasi yake ikachukuliwa na Aggrey Chiyangi na
msaidizi akawa Mumamba Numba.


Kwa sasa tayari Vandenbroeck amesaini mkataba wa
miaka mitatu kuinoa Simba akichukua nafasi ya Mbelgiji
mwenzake, Patrick Aussems ambaye hivi karibuni
alitupiwa virago.


Kawaida kwa makocha kufukuzwa au kutoongezewa
mkataba si jambo geni, pia kocha kufukuzwa au
kutopewa mkataba sehemu nyingine haina maana
hastahili kutofanya kazi sehemu nyingine.


Kawaida inaonyesha kocha mmoja anaweza kufanya
sehemu fulani akafanya vema, akihamia kwingine
akakwama. Mfano Vandenbroeck akiwa msaidizi alifanya
vizuri akiwa na timu ya taifa ya Cameroon ambayo
alikuwa sehemu kubwa ya kuingoza kubeba Afcon. Lakini
akiwa na Zambia, akashindwa hata kuisaidia timu kufuzu
tu!

Tayari ametua Simba ambao wana hamu kuu ya
mafanikio. Wanataka kuona timu yao inaendeleza ule
mwendo wa hadi robo fainali Afrika na kwa kuwa Simba
walishaonja mafanikio hayo, wana hamu kubwa ya
kupindukia kuhakikisha wanarudia na kufikia
walichokifanya msimu uliopita.


Vandenbroeck anaingia katika sehemu ambayo ina deni
kwake kwa kuwa kama atashindwa kusonga haraka,
Simba wana hamu kubwa na huenda wasiwe na subira
sana na asipoliangalia hilo, kuna uwezekano yale ya
Zambia, yakamtokea Simba.


Bado ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri hasa ukiangalia
namna wasifu wake binafsi ambao unaonyesha ni kocha
mchapakazi na ana nafasi ya kufanya vizuri pia kwa
kuwa ana mambo matatu makubwa. Kwanza ni mchezaji
ambaye alijitahidi kufika ngazi za mchezaji wa kulipwa,
kawa kocha msaidizi, kawa kocha mkuu tena katika
kiwango cha klabu na timu za taifa zikiwemo kubwa za
Zambia na Cameroon.


Upande mmoja wa timu hizo za taifa alifanikiwa, upande
mwingine alifeli. Hii ni nzuri kwa Simba kwa kuwa kocha
anayejua kuboronga ni nini, pia anakuwa bora sana
katika sehemu inayohitaji uokozi wa mambo.


Pamoja na hivyo, ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri au
kuwa imara barani Afrika kwa kuwa tayari ana uzoefu na
soka la bara hili.


Klabu:
Ukiachana na kwao Ubelgiji ambako alianzia akiwa
mchezaji hadi kuwa kocha, unaona Vandenbroeck
amefundisha timu za aina tatu. Timu za vijana, timu
kubwa na timu za taifa.

Unaona amekuwa kocha wa aina mbili, msaidizi ambaye
kwa mfumo wa Ulaya anabeba majukumu mengi zaidi
unapozungumzia kazi lakini pia amekuwa kocha mkuu
ingawa ni kwa muda mfupi.


Hii ni faida kwa Simba kutokana na Vandenbroeck kupitia
katika mapengo yote hayo maana yake ana uwezo wa
kupambana katika njia zote.


Mfano akiwa KV Mechelen ya kwao Ubelgiji alikuwa
kocha wa vijana, alipopata kazi kwa mara ya kwanza nje
ya nchi yake alikwenda Ugiriki ambako alikuwa kocha
msaidizi katika kikosi cha Fostiras ambacho baadaye
kilimpa nafasi ya kuwa kocha mkuu. Alipoondoka hapo
alijiunga na Niki Volos ya Ugiriki pia ambako pia akawa
kocha msaidizi na baadaye akawa kocha mkuu.


Mwisho aliamua kurudi kwao, Ubelgiji ambako alijiunga
na timu ya OH Leuven ambayo nayo alikuwa msaidizi na
baada ya miaka miwili akapata kazi ya kocha msaidizi
Cameroon, akafanikiwa kubeba ubingwa wa Afcon na
ndipo alipopata kazi Zambia.


Njaa:
Moja ya faida ambayo Simba wanaipata ni kwamba
Vandenbroeck atakuwa ni mtu mwenye njaa. Anarejea
tena kazini, safari hii akiwa tena kocha mkuu katika klabu
yenye hamu ya ushindi na mafanikio.


Simba wana kiu ya mafanikio, Vandenbroeck ana njaa ya
kufika mbali na tayari anajua kuhusiana na soka la Afrika.
Kama wataunganisha nguvu zao pamoja, kiu na njaa
zao, basi bila ubishi watakuwa na nafasi kubwa ya
mafanikio.


Bosi vigogo:
Kawaida aina ya makocha waliopitia mikononi mwa
makocha wenye njaa ya mafanikio. Mara nyingi huwa ni
wenye njaa isiyoisha kwa kuwa huwa wanatamani kufikia
au kuvuka walipofikia makocha wakubwa waliofanya nao
kazi.


Vandenbroeck amefanya kazi na makocha wengi
wakubwa hadi anafikia alipo sasa. Mfano, Broos Hugo,
huyu alifanya naye na ni kocha mkubwa ambaye
amefundisha timu kama Cameroon iliyobeba ubingwa wa
Afcon, lakini pia alipita Club Brugge na RSC Anderlecht
za Ubelgiji pia KRC Genk ambayo sasa anaichezea
Mbwana Samatta.


Kocha mwingine aliyefanya kazi ni Koster Adrie ambaye
alizifundisha klabu kubwa kama Ajax na PSV ya
Uholanzi, Club African ya Tunisia na timu ya taifa ya
Saudi Arabia.


Mchezaji:
Akiwa mchezaji pia amepitia timu kadhaa ambazo ni
kubwa kama Bergen ya Norway, Roda JC ya Uholanzi
ambayo imezalisha nyota wengi na unaona alicheza
karibu timu zote za vijana za Ubelgiji yaani U16, U17,
U19 na U21.


Kawaida makocha ambao wamecheza mpira wamekuwa
na uwezo mkubwa wa kung’amua mambo katika
kubadilisha kama kunatokea kitu.


Hivyo, njaa na kiu za pamoja za kocha na Simba
zikijumlishwa lazima zitazaa jambo jipya ingawa viongozi
na mashabiki wa Simba, wana jambo wanatakiwa
kujifunza. Kuna wakati mambo yanakwenda vizuri
mapema au yanakwenda yanaweza kwenda taratibu

hivyo, uvumilivu unatakiwa sana.

7 COMMENTS:

  1. yaani akaze buti kweli maana ligi imekuwa ngumu sana .. uchebe mwenyewe jasho lilimtoka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapo hawezi kudumu huyo Simba haina historia ya kukaa na makocha kwahiyo aje asafishe macho then atimuliwe

      Delete
  2. Kocha Bora gani msitudanganye angekuwa Bora asingekuja timu mbovu kama Simba huyo kocha njaaa tu

    ReplyDelete
  3. Tusiongopeane bwana mpira wa bngo hauendi hivyo kwa kuangalia cv mana kama cv tungeshachukua ubinga wa africa tayar hapa mfumo mbovu na kuwapangia makocha

    ReplyDelete
  4. Kocha amefika sehemu sahihi katika maisha yake ya kazi tangu aanze kufundisha mpira na huko kote alikopita alikuwa anahangaika ila Simba amefika nyumbani na Simba wamepata kocha sahihi. Kama aliaminiwa kupewa timu ya Taifa Zambia kama kocha wa Taifa hata kama hakufanya vizuri basi huyu jamaa ni kocha. Kuna taarifa yakwamba makocha wazawa wa Zambia walimfanyia figisu ili alishindwe kazi yake. Lakini hata ukiangalia matokeo ya mechi zake alizopoteza akiwa na kikosi cha chipolopolo basi hakupoteza kwa aibu. Unakumbuka Taifa stars chini ya Mkwasa tulivyozalilishwa na Algeria? Ujumbe kwa Selemani Matola kama anataka kutoka kwenye kazi yake ya ukocha basi huyu ndie pacha wake sahihi wa kumtoa ampe ushirikiano wa kutosha na uwe na mstaamilivu muda si mrefu takuja kujishangaa. Na kwa Wachezaji wa Simba hasa wazawa ni wakati wa kujipanga na kujiweka kwenye next level huu ndio wakati wa kumthibitishia kocha kwa vitendo kuwa mnaweza na mjiepushe na Majungu.

    ReplyDelete
  5. Acha ujinga wewe kandambili hata hamjuwi mnafanya nini zaidi ya kuvaa hayo madira ya kijani na njano eti kocha mbovu yule wenu mkwasa ndio kocha? Nyinyi sawa na kambare kakaeni huko matopeni hamna jipya safari hii mnapigwa mkono mfukuzane timu nzima

    ReplyDelete
  6. Uchebe ambaye mnamuona bora alipendekezwa na jopo la makocha. Kayuni na wenzake. Na huyu Vandenbroeck haohao wamehusika kwa weledi mkubwa.waulizen hata kwa siri kwa nini hao makocha weledi walimpendekeza huyu kocha. Simba oyee

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic