December 27, 2019



JUMA Abdul, nohodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa kulazimisha sare mbele ya Mbeya City hawajakata tamaa watapambana kutibua rekodi ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine.

Yanga ililazismisha sare ya bila kufungana mchezo wao wa tisa leo itamenyana na Prisons ambayo mpaka sasa haijapoteza hata mchezo mmoja kwenye mechi zake 12 ilizocheza ilishinda mechi nne na ililazimisha sare mechi 8.

Abdul amesema kuwa mashabiki wa Yanga wasiwe na presha juu ya kikosi chao kwani matokeo yanayotokea yanawahusu wote na hawajakata tamaa ya kupambana.

“Haina maana kwamba tutaendelea kupata sare hapa hii ni ligi na tuna mechi nyingi za kucheza, mashabiki wasiwe na presha juu yetu tutapambana kupata matokeo na inawezekana kutibua rekodi za wapinzani wetu.

“Rekodi siku zote zinawekwa ili zivunjwe nina amini tutafanya kweli kwa wapinzani wetu kutokana na kujifunza kwa makosa ambayo tumeyafanya,” amesema Abdul. 

Mchezo wa leo utachezwa uwanja wa Samora Iringa badala ya Sokoine ambao umeharibiwa na tamasha lililofanywa hivi karibuni kwenye sehemu ya kuchezea.

2 COMMENTS:

  1. Kila la kheyr watani jitahidini sana maana mwaka huu hakuna timu nne

    ReplyDelete
  2. Ila Tanzania kwa vimbwanga utakuta mahojiano yamefanyikia Dar wakati timu ipo mbeya na Juma Abdul sio sehemu ya waliopo mbeya🤗

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic