December 27, 2019


BONIFACE Pawasa, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Beach Soccer ambao ni mabingwa wa Copa Dar es Salaam amesema kuwa walistahili kutwaa ubingwa huo kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

Tanzania ilishinda mabao 6-3 mbele ya Burundi kwenye mchezo wa mwisho uliochezwa viwanja vya Coco Beach jana Desemba 26.

Akizungumza na Saleh Jembe, Pawasa amesema kuwa mashindano yalikuwa bora na kila timu ilionyesha ushindani.

"Tulijiandaa kupata matokeo chanya licha ya kupoteza mchezo wa kwanza mbele ya Uganda kwa kufungwa mabao 2-1 wengi walipoteza imani kwetu na walishindwa kujitokeza kwa wingi mwisho wa siku tumefikia malengo yetu," amesema.

Timu tano zilishiriki mashindano hayo ambazo ni pamoja na Burundi mshindi wa tatu, Malawi, Uganda mshindi wa pili, Seychells iliyopewa tuzo ya timu yenye nidhamu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic