BONIFACE Mkwasa, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kuna tatizo kwa waamuzi wa Bongo jambo ambalo limemkosesha pointi tatu mbele ya KMC.
Yanga jana imekubali sare ya kwanza mbele ya KMC ambayo msimu uliopita ilifungwa nje ndani mechi za ligi kuu na kuacha poiti sita kwa Yanga.
"Tulitengeneza nafasi nyingi na tulishindwa kuzitumia kwani uwezo wetu umeonekana ndani ya uwanja.
"Waamuzi wanamaamuzi yao ila kutakuwa na ulazima wa kuangalia kile ambacho wanakifanya hasa kwenye mechi hizi zenye ushindani mkubwa," amesema.
Yanga jana ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na KMC uwanja wa taifa, bao lao la kwanza lilifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 73 huku lile la KMC likifungwa na Abdul Hilary kwa mkwaju wa penalti dakika ya 90+4.
Malalamiko Kwa kila baada kufungwa au kutoka suluhu ilikuwa ndio silaha kubwa ya kocha Zahera ya kujitetea
ReplyDeleteHii ndio bongo soccer na shida ya kuingia na matokeo mfukoni hata ndanda,alliance na JKT Tanzania nao walilalamika kuwa waamuzi wamempendelea mkwasa
ReplyDeleteRefa angekuwa muadilifu jana KMC wsmeshinda.Aliwabeba Yanga bila aibu.
ReplyDeleteNilitegemea kocha wa KMC ndio amlalamikie refa baada ya kuinyima timu yake penati ya wazi kabisa. Pia refa alipaswa kumtoa nje kwa kadi nyekundu Kelvin Yondani kwa faulo yake dhidi ya Salum Kabunda iliyosababisha penati na bao la kusawazisha la KMC. Yondani tayari alikuwa na kadi ya njano. Kifupi, refa aliwabeba Yanga.
ReplyDeleteKwa kweli sikutegemea Kocha wa Yanga (Mkwasa) aongee, timu yake jana ilipoteza pointi kwa sababu ya uwezo wake mdogo wa kuusoma mchezo na kufanya maamuzi!
ReplyDeleteTimu yake ilielemewa kwenye kiungo kwa uamuzi wa kumchezesha Sonso badala ya Balama kiasi kwamba katika kipindi cha kwanza Yanga hawakufanya shambulizi lolote la maana, alipofanya mabadiliko (dk ya 71) Yanga walibadilika.
Kosa la 2, Sadney alishindwa kabisa kucheza lkn Kocha alimwacha kwa kipindi kizima bila kumtoa na kumweka Ngasa ambaye angeshirikiana na Kaseke kuongeza kasi ya mchezo.
Kosa la 3, rasta Jafar ngoma ilimuelemea tangu kipindi cha kwanza Kocha akamwacha hadi mwisho, kocha hakuiona ile penalti aliyotaka kuisababisha?
Kosa la 4 ni kuwaruhusu wachezaji 3 wote wa kiungo kwenda Zanzibar heroes wakati akijua hakuna mbadala.
Kocha asisingizie ratiba na nina mshauri Mkwasa asitake kujenga uhalali wa kuwa kocha wa kudumu; uwezo wake bado mdogo. Akumbuke akiwa kocha wa Taifa stars alivyolishwa 7 Algeria!