December 3, 2019


Nahodha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Papy Tshishimbi, amepanga kukutana na mabeki wa timu hiyo kwa ajili ya kufanyia kazi changamoto ya kuruhusu mabao kila mchezo na anaamini watarekebisha tatizo hilo haraka.

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba utakaopigwa Januari 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga katika mchezo wa jana wa ligi iliruhusu bao la nane tangu kuanza msimu huu katika suluhu ya 1-1 dhidi ya KMC. 

Yanga ina wastani wa kufungwa bao moja katika kila mchezo, hali inayofanya wakutane kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuhakikisha hawaruhusu mabao kwenye michezo ijayo.

Tshishimbi alisema kuwa kaimu kocha wao Charles Mkwasa anawaelekeza jinsi ya kuzuia ili wasifungwe, lakini bado wanaendelea kuruhusu mabao, hivyo hawataki kuona hilo likiendelea.

“Kocha anatuelekeza jinsi ya kuzuia ili tusifungwe lakini sisi kama wachezaji pia tunazungumza turekebishe makosa haya mnayoyaona yakitokea katika michezo yote ya ligi tuliyocheza.

“Hivyo, tumepanga kukutana mabeki na viungo wakabaji kwa ajili ya kuweka mikakati hiyo ya kutofanya makosa ya kizembe yatakayotufanya turuhusu mabao kizembe golini kwetu,” alisema Tshishimbi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic