January 9, 2020


INAELEZWA kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ambaye anakipiga katika Klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta, wikiendi iliyopita alitua nchini England kwa ajili ya masuala ya usajili.

Norwich City inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini England iliripotiwa kuweka dau linalofikia pauni milioni 11 (Sh bil 33), huku thamani ya mchezaji huyo ikiwa ni kiasi cha euro milioni 12 ambazo ni sawa na pauni milioni 10 (Sh bil 30).

Baba mzazi wa mchezaji huyo, Ally Samatta, aliliambia Championi Jumatano kuwa, ni kweli mtoto wake ameenda England ambapo ameitwa na wakala wake, Scops Global Sports, kwa ajili ya kwenda kuzungumzia masuala ya usajili lakini aliongeza kuwa, kwa sasa vita ya usajili kwa mtoto wake imeongezeka kutokana na timu nyingine ya nchini humo, West Ham United, kuingia vitani katika kuwania saini ya Mtanzania huyo.

“Ni kweli Norwich wanamtaka Samatta na ameenda England kwa kuwa aliitwa na wakala wake kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusiana na usajili wake, lakini vita imezidi kuwa kubwa, kwa sababu timu ya West Ham nayo inamhitaji,” alisema mzee Samatta.

Hata hivyo, jana mtandao wa Ligi Kuu ya England uliweka picha ya Samatta ukionesha kuwa ni mchezaji wa ligi hiyo.

Tangu msimu uliopita hadi sasa katika mashindano yote, Samatta amecheza michezo 71, amefunga mabao 42, huku akiwa ametoa asisti nane.

Wakati huohuo, taarifa za jana zilisema kwamba Simon Msuva anayecheza Diffa El Jadida ya Morocco anajiandaa kujiunga na Benfica ya Ureno.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic