January 7, 2020


NAHODHA wa Simba, John Bocco leo ameongoza kikosi chake kushinda mabao 3-1 dhidi ya Zimamoto kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi.

Simba ilianza kupata bao la kwanza dakika ya nne kupitia kwa Bocco aliyemalizia pasi ya Ibrahim Ajibu kabla ya bao la pili kuandikwa na Sharaf Shiboub dakika ya tisa na Zimamoto waliandika bao la kufutia machozi dakika ya 28 kupitia kwa Ahmad.

Kipindi cha kwanza kilikamilika kwa Simba kuwa mbele kwa mabao 2-1 na waliongeza bao la tatu na mwisho dakika ya 53 kupitia kwa Ajibu akimalizia pasi ya Shiboub.

Sasa Simba inatinga hatua ya nusu fainali itamenyana na bingwa mtetezi Azam FC.

1 COMMENTS:

  1. Leo roho ilikua inadunda sana,nilifikiri wale watatufanya kama yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic