January 4, 2020


SELEMANI MATOLA Matola aliyezaliwa Aprili 24, 1978 ni zao la Simba kutokana na kuitumikia timu hiyo kwa muda mrefu kuanzia uchezaji hadi ukocha.

Alianza kuitumikia Simba akiwa mchezaji mwaka 1999 ambapo alidumu katika kikosi hicho kwa misimu saba hadi 2005 alipotimkia Super Sport United ya Afrika Kusini  mwaka 2006 na kurejea mwaka 2008.

Matola ni miongoni mwa makocha wazawa ndani ya Simba waliowahi kufanya vizuri katika kikosi hicho kwa vipindi ambavyo amewahi kuitumikia timu hiyo kuanzia Simba B hadi timu ya wakubwa akiwa kocha msaidizi.

UZOEFU WA MATOLA

Matola alianza kuitumikia Simba tangu mwaka 2011 akiwa kocha wa vijana wa Simba B ambapo alifanikiwa kushinda mataji matatu katika timu hiyo ambayo ni kombe la vijana, Kombe la Mapinduzi na Super 8.

Pia alipata nafasi ya kuifundisha Simba kwa nyakati tofauti kama kocha msaidizi chini ya kocha Zdravko Logarusic raia wa Croatia msimu wa 2013/14, Patrick Phiri raia wa Zambia mwaka 2014 na Goran Kopunovic raia wa Serbia mwaka 2015 na sasa chini ya Sven msimu wa 2019/20.

HISTORIA YAKE YA KUIFUNGA YANGA

Wakati alipokuwa akiifundisha Lipuli msimu uliopita, alikuwa miongoni mwa makocha ambao waliokuwa wakizitesa timu kongwe za Simba na Yanga, nadhani ni kutokana na uzoefu wake wa kuzijua timu hizo.

Kati ya michezo aliyocheza dhidi ya Yanga msimu uliopita katika mzunguko wa kwanza Lipuli ilifungwa bao 1-0 alilofunga Heritier Makambo dakika ya 10 kwenye Uwanja wa Taifa, Lipuli ililipiza kisasi kwa kuifunga Yanga bao 1-0 lililofungwa na Haruna Shamte dakika ya 20 kwenye Uwanja wa Samora.

Alifanikiwa kuitoa Yanga kwenye michuano ya Kombe la FA katika hatua ya robo fainali msimu uliopita, hivyo kuonekana kuwa mbabe wa Yanga.

Vilevile katika mchezo wa kirafi ki waliocheza wakiwa wanajiandaa na msimu mpya wa 2019/20 walipokutana akiwa na Polisi Tanzania walishinda kwa mabao 2-0, vilevile alitoa sare ya mabao 3-3 katika mchezo wa ligi akiwa hapohapo Polisi Tanzania. Hivyo, ana uzoefu mkubwa wa kuwafunga Yanga katika mchezo huo kutokana na historia yake.

KUHUSU MKWASA

Mkwasa  ambaye amezaliwa Aprili 10, 1955 mjini Morogoro alianza kuitumikia timu hiyo mwaka 1979 ambapo alidumu kwa miaka 11 hadi alipoamua kustaafu mwaka 1989.

SAFARI YA UKOCHA YANGA

Alianza kuinoa Yanga mwaka 1991 akiwa chini ya Syllersaid Mziray ambaye kwa sasa ni marehemu. Mwaka 2001 alikuwa klabuni hapo aliporithi mikoba ya kocha Raoul Jean Pierre Shungu wa DRC, alifanikiwa kuifi kisha hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa na Mamelodi Sundwons ya Afrika Kusini baada ya kufungwa 3-2 ugenini na kutoa sare ya mabao 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mwaka 2013 alirudi tena Yanga chini ya Hans Pluijm raia wa Uholanzi akiwa msaidizi kabla ya kuondoka mwishoni mwa msimu kuelekea Saudi Arabia katika timu ya Al Shoolai.

Mkwasa alirejea kwa mara nyingine Desemba, mwaka 2014 pamoja na Plujim kuchukua mikoba ya Mbrazili, Marcio Maximo na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na kuifi kisha Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika ambapo ilitolewa na Etoile du Sahel ya Tunisia.

Hivyo, kipindi chote hicho alichokuwa na timu hiyo ameshawahi kuwafunga wapinzani wao mara kadhaa, ni matumani ya Wanayanga kuwa atawavusha vyema katika mchezo huo kutokana na uzoefu wake kwa kuzijua vyema fi tina za Simba na Yanga. Pamoja na takwimu hizo, kilichobaki ni matokeo ya uwanjani, wachezaji wanasubiriwa kuandika rekodi mpya ndani ya dakika 90.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic