January 15, 2020


KIUNGO bora ndani ya klabu ya Simba msimu wa mwaka 2018/19 James Kotei ambaye alitimkia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini amekubaliana kuvunja mkataba na klabu hiyo huku akisema kuwa hakuwa na furaha ndani ya timu hiyo.

Kaizer Chief wamefikia hatua hiyo baada ya kumpata mbadala wake kutokana na Kotei kutokuwa na nafasi ndani ya kikosi hicho.

Kotei amesema kuwa alikuwa hapati namba kikosi cha kwanza na hakuwa na furaha ndani ya timu hiyo kutokana na hali hiyo kwani furaha yake ipo kwenye kucheza.

"Sikuwa na furaha kwa kuwa nilikuwa sipati namba, natarajia kupata timu hivi karibuni ila sijazungumza na Yanga jambo lolote kuhusu wao kuhitaji saini yangu," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic