January 29, 2020

CHAMA cha mpira wa Kikapu Marekani (NBA) kimeahirisha mchezo wa Ligi ya NBA kati ya Los Angeles Clippers uliopangwa kufanyika usiku wa kuamkia leo Jumatano baada ya kutokea kwa kifo cha gwiji wa mchezo huo nchini humo, Kobe Bryant.

Kobe aliyecheza NBA kwa miaka 20 akiwa na LA Lakers alifariki Jumapili iliyopita kwa ajali ya helkopta iliyoanguka akiwa na mwanawe Gianna na watu wengine Saba ambao wote walifariki kwenye ajali hiyo iliyotokea Calabasas, California, Marekani.


Taarifa iliyotolewa na LA Lakers, ilisema : " Mechi kati ya Los Angeles Lakers na Los Angeles imeahirishwa itapangiwa siku nyingine.


Watu wengi duniani wameumia na Msiba huo ambapo mchezaji anayefanya vema kwenye Kikapu Kwa sasa, LeBron James amesema kuwa: " Nimeumia moyoni kwa kumpoteza kaka yangu,".


Timu mbalimbali duniani zimetumia mitandao ya kijamii kuandika namna zilivoguswa na msiba huo ikiwa ni pamoja na wachezaji pia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic