Kocha wa klabu ya Yanga, Luc Eymael ameonesha kutofurahishwa na waamuzi wa mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC uliopelekea kufungwa bao 1-0 juzi Jumapili, Januari 19
Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, umeshuhudia Yanga ikipoteza mchezo wa pili mfululizo chini ya kocha huyo katika ligi kuu.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Eymael amesema kitendo akichofanyiwa na mwamuzi wa kati cha kukataa kumpa mkono amekitafsiri kama ni ubaguzi dhidi yake.
"Nataka nizungumze suala la waamuzi, kweli ile ni kadi nyekundu lakini kabla mchezaji wa azam hajafanyiwa madhambi alimvamia mchezaji wa Yanga, mwamuzi wa pembeni alikuwepo pale lakini akasema hakuona kitu. Mwambuzi akaja kwangu kunipa kadi ya njano nikampa mkono lakini akaukataa, kwanini mko hapa, ni kwasababu mimi ni mzungu?, ni ubaguzi dhidi ya watu weupe?, kiukweli nimefadhaika sana", amesema Luc
"Kwa hali hii ilivyo, ninafikiria juu ya hatma yangu hapa, nitaongea na kamati juu ya hatma yangu. Siridhishwi na kinachoendelea hapa, sizungumzii juu ya Azam FC bali nazungumzia juu ya vitu hivi vingine kwenye mchezo", ameongeza.
Kuhusiana na mchezo kiufundi, kocha Eymael amesema kuwa bahati haikuwa upande wao katika mchezo huo, kwani walicheza vizuri kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi za kutosha lakini hazikuzaa matunda na mwisho wakafungwa bao ambalo amesema hakuelewa limetokeaje.
Kocha huyo sasa amepoteza mechi ya pili mfululizo katika ligi, akifungwa jumla ya magoli manne, huku timu yake ikiwa haijafunga bao lolote.
Darkness cannot drive out darkness, only light can do that. Patience is bitter, but it's fruits are sweet
ReplyDeleteQuotation
HAPA KUNA TATIZO TENA KUBWA SANA,YANGA MSIPOANGALIA HUYO MDHAMIN WENU ATAJITOA MAPEMA SANA 1:KOCHA MLIEMPA DHAMANA YAKUSIMAMIA TIMU ANAONEKANA MAPEMA KABISA KWAMBA HANA UWEZO WA KIMBINU WAKUMSHINDA MWINYI ZAHERA HIVYO MNATAKIWA MFANYE TATHIMIN YA GHARAMA MNAZOMPA KOCHA WA SASA NA AINA YA MATOKEO MNAYOYAPATA KAMA HAVIENDANI HAPO LAZIMA KUTAFUTA SULUHU YA KUDUMU KUONDOA HILO TATIZO,KWA ALIVYOKUA ANAJITOA MWINYI ZAHERA KABLA HATUJAENDA KUANGALIA UBORA WA KIKOSI HAKUSTAHILI KUFUKUZWA.2:WAKATI YUPO MWINYI ZAHERA KIKOSI CHA YANGA HAKIKUA BORA KAMA KILIVYO SASAHIVI,KWA MAANA HIYO KINAPASWA KUA NA MATOKEO BORA ZAID KULIKO YA KIPINDI CHA ZAHERA NA KAMA INAENDA TOFAUTI PIA FANYENI TATHIMIN NA MTAFUTE SULUHU YA KUDUMU YA TATIZO HILO.MAONI NA USHAURI MKWASA ANGEENDELEA KUKAIMU NAFASI HII MPAKA PALE KOCHA MWENYE UWEZO WA KIMBINU ANGEPATIKANA MAANA YAKE INAONEKANA YANGA MMEKURUPUKA KWENYE HILI SUALA.3:KAMA ITASHINDIKANA NI BORA ZAHERA ARUDI YANGA KULIKO UJINGA UNAOENDELEA HAPO JANGWANI,JARIBUNI KUONYESHA UTU KWA ZAHERA KWA KILE ALICHOKUA ANAIFANYIA YANGA INAWEZEKANA NAFSI YAKE INA KINYONGO SASA HAPA KIDOGO TUNAWEZA TUSIFIKE POPOTE,SITAKI KUANIKA ALICHOKIFANYA ZAHERA KWA YANGA KWANI KILA MJA MWENYE AKILI NA ALIEKUA ANAFUATILIA MPIRA ANAJUA LEO HII MNAMFUKUZA IKIWA MAZINGIRA NDIO YALIYOKUA MABOVU KWENYE CLUB.4:YANGA NI TIMU KUBWA SANA NA MARA NYINGI SANA IMEKUA HAIKOSEI KWENYE SUALA LA USAJILI,IMEKUA IKISAJILI WACHEZAJI WENYE MAPENZI NA TIMU NA SIO WAPIGA PESA TOFAUTI NA MAJIRANI ZETU ILA SAFARI HII KIDOGO NAONA KAMA TUMEBUGI,NASEMA HIVI KWASABABU INAONEKANA WACHEZAJI WENGI WALIOSAJILIWA MSIMU HUU WA DIRISHA DOGO SIO WALE TULIOWAZOEA,TENA INAONEKANA VIWANGO VYAO NI DUNI NA VYA CHINI KULIKO AKINA MOLINGA NA PS2 PATRICK SIBOMANA KWA MAANA HIYO HAWATAKUA NA MCHANGO MKUBWA KWENYE TIMU IKIWEZEKANA PIGA CHINI ALAFU MSIKILIZENI ZAHERA KUPITIA GSM APENDEKEZE WACHEZAJI,HONGERA KWA WACHEZAJI WA NDANI HAMJAKOSEA HATA KIDOGO WACHEZAJI WA NDANI WOTE MLIOWASAJILI NI WALE WANAOJITOA NAKUIPENDA YANGA ILA HAPO KWENYE KIMATAIFA HAKUNA KITU KWAKWELI JARIBUNI KUANGALIA IKWEZEKANA TIMUA WACHEZAJ RUDISHA ZAHERA GSM WAMTENGENEZEE MAZINGIRA KOCHA ALAFU MTAKUJA KUTOA MREJESHO HAPA.ZAHERA NI KOCHA TENA KOCHA BORA WA MUDA WOTE.
ReplyDelete