January 4, 2020


HARUNA Niyonzima, kiungo wa Yanga mwenye ufundi wake uwanjani, tayari ameshakabidhiwa viatu maalum tayari kwa kuhakikisha anawagaragaza walinzi na viungo wa Simba leo Jumamosi.

Simba anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Yanga leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, ni mara ya kwanza timu hizi zinakutana msimu huu, mchezo wao wa mwisho Simba ilishinda bao 1-0.

Niyonzima ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili ambalo lipo wazi tangu Desemba 16, mwaka jana na utafungwa Januari 15, mwaka huu.

Niyonzima alitua nchini juzi Alhamisi akitokea kwao Rwanda na Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kiungo huyo amekabidhiwa vifaa vyake ikiwemo viatu maalumu tayari kwa kuwamaliza Simba leo.

“Niyonzima tayari ameshakabidhiwa viatu vyake kwa ajili ya mchezo wa kesho (leo) pamoja na jezi ikiwa ni utaratibu wa klabu hata kama mchezaji amekuja na vifaa vyake, hivyo ni lazima apewe vifaa vipya, hata wachezaji wengine wapya wamepewa baada ya kutua,” alisema Bumbuli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic