LICHA ya kutoka kwenye majeraha ya goti, kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema anaona wazi kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, John Bocco anapiga hat trick safi dhidi ya Yanga leo.
Kama Bocco atafunga hat trick leo pale Uwanja wa Taifa, basi ataifikia rekodi ya Kibadeni ya kufunga hat trick dhidi ya Yanga ambayo aliiweka Julai 19, 1977.
Kibadeni alifunga hat trick hiyo na kuisaidia Simba kushinda mabao 6-0, alitupia mabao yake dakika za 10, 42 na 89. Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Jumanne Hassan ‘Masimenti’ dakika za 60 na 73 na lingine lilikuwa la kujifunga la Selewa Sanga wa Yanga dakika ya 20.
Kibadeni alisema kuwa, anaona wazi Bocco ana nafasi kubwa ya kufunga mabao matatu licha ya kuwa ametokea kwenye majeraha yaliyomfanya akae nje kwa muda mrefu.
“Nampa nafasi kubwa Bocco kuweza kufunga mabao matatu katika mchezo huo kwani kiwango chake kipo vizuri licha ya kutoka majeruhi, hivyo akijitahidi atafunga mabao matatu,” alisema Kibadeni na kuongeza:
“Simba ipo vizuri sana kwa sasa tofauti na Yanga ambayo kikosi chake sio kipana kama Simba, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kuibuka washindi zaidi ya bao moja katika mchezo wa kesho (leo).
0 COMMENTS:
Post a Comment