MEDDIE
Kagere, mshambuliaji wa Simba ameundiwa jeshi la kazi ndani ya Yanga litakalomzuia
asilete hatari ndani ya lango lao kwenye mechi ya kesho litakalokuwa chini ya
Metacha Mnata ama Farouk Shikalo.
Kagere
mwenye mabao tisa ndani ya ligi pamoja na asisiti mbili aliwaachia maumivu
Yanga msimu wa 2018/19 walipokutana Uwanja wa Taifa kwa kufunga bao la ushindi
lililowapotezea kasi ya kulisaka taji la ligi Simba iliposhinda bao 1-0.
Akizungumza
na Championi Jumamosi, nahodha msaidizi wa Yanga, Juma Abdul ambaye ni beki
aliyecheza jumla ya mechi saba kati ya 11 ndani ya kikosi hicho alisema kuwa
wanatambua namna ya kupambana na washambuliaji wa timu pinzani.
“Tumefundishwa
mbinu nyingi na mechi ambazo tumecheza zimetuongezea hali ya kujiamini tupo
sawa na tutapambana kufanya kazi ya kweli uwanjani, ni jeshi la kazi
litakalozuia mipango hasa ukizingatia ligi ina ushindani.
“Kikubwa
ambacho kinatupa nguvu ya kujiamini ni maandalizi pamoja na mashabiki hivyo
tunaamini kazi yetu itakuwa kwa vitendo ndani ya uwanja, tunawaomba mashabiki
wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” alisema Abdul.
Mtamchunga Kagere watawatungua wengine .Nä hiyo ndio plani ya leo.Fungukeni please wacheni kubana miguu .
ReplyDeleteMwandishi anasema mechi ya kesho!!! Ni kesho au jioni hii?
ReplyDelete