Inaelezwa kuwa beki aliyewahi kuichezea Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' ameondoka kunako klabu yake ya LA Galaxy II ya Marekeni.
Taarifa zinasema kuwa wakala wake Alex Morfaw amesema beki huyo ameondoka La Galaxy ya Marekani kutokana na Klabu hiyo kutomhakikishia nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha kwanza kwa msimu huu.
Wakala Alex amedai kuwa muhimu kwao ni Ninja kupata nafasi ya kucheza na kuendelea kuimarika zaidi.
Kwa sasa wamepata nafasi ulaya na wanasubilia kibali cha kufanya kazi kwa ajili ya kuanza changamoto nyingine mpya.
Dogo aache papara hasa sehemu za kukaba kwa kutumia akili akishindwa aache wenzake watakaba....
ReplyDelete