January 27, 2020

7 COMMENTS:

  1. Mghana na shoo zake ila akili yake yote ipo Simba. Na ni kama kweli mchezaji basi atachukuliwa tu na Simba wakati ukifika hakuna mjadala juu ya hilo. Ila Yanaga ni malimmbukeni wa kutupwa.Mcezaji kacheza mechi mbili tu,makelele kama makasuku yaani kama vile kuwachukulisha ubingwa tayari.Morison anaonekana mchezaji Yanga kwakuwa yanga hawana wachezaji wa maana ndani ya kikosi chao. Licha ya ubora wote unaopigiwa kelele wa Morrison basi hamfikii khasan Dilunga hata robo yake.

    ReplyDelete
  2. Kama kocha wa Simba kapata first eleven basi sawa,ila inawezekana kama kapata kikosi cha MAUAJI basi itakuwa ndani ya ligi ya Bongo, ila kwa kikosi cha Africa basi Simba bado kazi wanayo ya kukiimarisha kikosi chao na sababu kubwa ya kusema Simba bado hawana kikosi cha kushindana Africa ni hivi. Mpira ni beki bana na kama huamini kawaulize Liverpool.Baada ya kuteseka na kuzalilika kwa miaka kadhaa Liverpool uengereza na barani ulaya ndipo alipokuja Mjerumani na moja ya kitu alichokifanya alipofika tu Liverpool ni kununua beki ghali kuliko beki wote ndani ya primier league na Watu wengi walimuona kama mgonjwa wa akili ila historia ya mpira wa miguu duniani inajieleza wazi yakuwa ili timu kupata mafanikio basi lazima iwe na mfumo uliokamilika wa kujilinda unaochagizwa na mabeki imara. Simba kama ingizo jipya la wabrazili halikuweza kufunika uwezo wa mabeki waliosababishia Simba kupata vipigo vya aibu Africa pamoja na kutolewa na UD SONGO basi simba kwenye CAF championship aibu hiyo itawakuta tena msimu unaokuja kama watafanikiwa kuiwakilisha nchi Africa. Simba wanafanya mzaha au tuseme ubahili katika kutafuta beki wa kati aliekamilika kwenye backline yao kwa kipindi.kirefu sasa. Kama beki ya Simba inafungwa magoli mepesi na mtibwa au mwadui au hata timu iliyotembeza bakuli kununua wachezaji kama YANGA? Itakuwaje kwa timu kama Tp Mazembe au National Ahly au Esperence? Sisemi kuwa mabeki wale wa Simba hawafai ila ukweli uliodhahiri kabisa kumtegemea wawa na Pacha wake Erasto Nyoni na kutengemea kwenda kufanya maajabu na kuvuka malengo Africa ni kujidanganya mchana kweupe.Tunajua Simba walifanya usajili wa mabeki kazaa wapya wakuja kuimarisha beki yao ila sina uhakika kama wamekizi malengo? Na tatizo kubwa ni beki wa kati aliekamilika atakaeituliza backline zima ikiwezekana kupanda kwenda kufunga magoli muhimu hasa kwenye mipira ya kona,Mtu kama huyo kwa Simba bado ni donda ndugu. Apewe muda kocha na benchi lake la ufundi ila tatizo la Simba linafahamika wazi na siku nyingi asije kocha huyu na benchi lake la ufundi kuja kubebeshwa zigo kwani kiuhalisia halimuhusu. Kocha huyu wa Simba yupo profession zaidi katika kazi yake unamuona kabisa ila juhudi za dhati zifanyike mapema kumsaidia kuindaa timu kwa ajili ya Caf championship na moja ya eneo la kulijadili zaidi ni eneo la ulinzi kwakuwa ndiko Simba imipofeli zaidi kunako mashindano yaliyopita.

    ReplyDelete
  3. Simba wangekua na pesa wange mbakiza Okwi,
    MO ndio roho yenu Aki watisha wote akili hazikai sawa.

    ReplyDelete
  4. Nina uhakika Deo Kanda akipona na Luiz akipata ITC yake wataingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha Simba. Suala la mabeki angalao wawili wanaojua kukaba na wenye kasi ya kukimbizana na washambuliaji ni muhimu sana kwa Simba, hasa watakapokwenda kwenye michuano ya kimataifa. Wanapaswa pia kusajili mshambuliaji mmoja wa kati mwenye uwezo mkubwa kuliko Kagere na Bocco. Wakifanya hivyo watakuwa hawakamatiki. Katika eneo la kiungo Simba ina wachezaji bora pengine kuliko timu yoyote Afrika Mashariki na Kati.

    ReplyDelete
  5. Ni ukweli usiopingika kuwa Simba inahitaji mabeki wawili wa kati wenye nguvu kama Lamine Moro/Yakubu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yakubu na lamine bado ni sawa tu na wawa na nyoni simba kama simba hakuna beki yeyote ndani ya ligi hii ataeweza kutumikia nafasi hiyo na kuikomboa timu mechi za away hasa Champions League labda watafute beki imara kutoka nje africa mashariki

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic