January 25, 2020

MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC, Gerald Mdamu amesema kuwa akipata nafasi leo ya kuanza dhidi ya Simba atapambana kuipa ushindi timu yake ili isonge hatua ya 16 kwenye hatua ya kuwania Kombe la Shirikisho utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.
Mdamu aliifunga Simba walipokutana kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara zilipokutana Uwanja wa Kambarage na leo watakutana na Simba Uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa hatua ya 32 bora.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mdamu amesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Simba utakuwa mgumu ila wamejipanga kupata ushindi ili kufikia malengo waliyojiwekea.
“Tumepangwa na Simba na tunatambua kwamba wana hasira kutokana na kwamba tuliwafunga kwenye mechi yao tulipokutana nao kwenye mchezo wa ligi, tutapambana kushinda mashabiki watupe sapoti,” amesema.

1 COMMENTS:

  1. Siku zote huwezi kushindana na mtu aliepanga kukushinda,simba mnapaswa kua makini sana kwenye asfc isije ikawasababishia majeraha mkajashindwa kutetea ubibgwa wa ligi kuu,kwasababu mwadui anakuja na matokeo yake basi mpisheni apite ili sisi tubaki kwenye ligi kuu.ni ushauri tu lakini ahsanteni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic