January 11, 2020


Mlinda mlango wa KMC inayoshiriki Ligi Kuu Bara na Timu ya Taifa (Taifa Stars), Juma Kaseja, amesema anatarajia kurejea tena uwanjani mapema mwezi ujao.

Kaseja alifanyiwa operesheni ya goti la mguu wa kulia hivi karibuni, baada ya kubainika kuwa na uvimbe, siku chache kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Chalenji Desemba mwaka jana.

Kaseja alisema anaendelea vema na tayari ameanza mazoezi 'maalumu' chini
ya madaktari wa Taifa Stars.

Kaseja alisema anamshukuru Mungu, amewahi kupata matibabu kabla ya tatizo lake kuwa kubwa na hivyo anatarajia kurejea uwanjani katika mechi za Ligi Kuu Bara hivi karibuni.

“Namshukuru Mungu niko vizuri, sina maumivu, na nimeshaanza mazoezi maalumu, kurudi uwanjani kamili hadi Februari," alisema

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic