January 11, 2020


Imeripotiwa kuwa Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck ameitaka bodi ya klabu hiyo kufuta makubaliano ya mkopo na Klabu ya Coastal Union kuhusu Beki wa Kati Bakari Nondo Mwamnyeto. 

Taarifa inasema kuwa Sven ameitaka bodi hiyo isajili beki wa kati mmoja na mshambuliaji mmoja ili kuimarisha kikosi chake.

Tayari Simba ilishamsajili Nondo na kumtoa kwa mkopo wa miezi sita Coastal Union.

Kocha huyo ambaye ameiwezesha Simba kutinga fainali ya Mapinduzi CUP baada ya kuiondoa Azam FC, amesema Mwamnyeto anatakiwa ajiunge na kikosi kufikia mwezi wa sita akiamini atakuwa tayari ameshapata uzoefu.

1 COMMENTS:

  1. Thanks coach kama umeliona hilo ni vizuri sana,jana simba ingefunga magoli mengi sana ila ukweli ni kwamba pale mbele bado kuna mapungufu pengo la okwi kamwe halijazibwa,lingefanyiwa kazi kwa haraka kabla ya kimataifa kuanza kuanza kutimua vumbi,hii ingesaidia sana kwa timu kupata matokeo mazuri.all in all hongera kwa kusonga mbele hatua ya fainali maana haikua kazi nyepesi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic