January 3, 2020


JOTO la mechi ya watani linazidi kupanda kwa sasa ambapo kila mchezaji na benchi la ufundi wa timu hizi mbili hawana kingine wanachofikiria kwa sasa zaidi ya kuona ni namna gani watatoka baada ya dakika tisini kupita Januari 4,2020.

Leo, Januari 3 yammebaki masaa kadhaa kabla ya watani hawa kumenyana pale uwanja wa taifa na miongoni mwa wachezaji ambao wanakipiga Simba yupo beki mpya, Gadiel Michael ambaye alijiunga na Simba akitokea Yanga kwa kadandarasi ya miaka miwili anatambua joto lake kwa sasa.

Championi Jumatatu limefanya mahojiano naye kuhusu namna anavyokiona kikosi chao cha Simba pamoja na maandalizi kuelekea kwenye mechi hiyo pamoja na nyingine ambazo zinawahusu wakiwa ni mabingwa watetezi huyu hapa anaanza:-

“Nimekuwa kwenye masiha ya soka la ushindani kwa muda mrefu na inanifanya nakuwa bora siku zote kutokana na muda ambao nimecheza jambo ambalo linanifanya nizidi kupambana siku zote nje na ndani ya uwanja.

Kipi kinakufanya usichuje?

“Nidhamu katika kila jambo ambalo ninalifanya na kutambua nini ambacho ninakitaka na kwa wakati gani ambao ninafanya.
“Katika kila ambacho ninakifanya ninamtanguliza Mungu ambaye yeye ni mpaji wa yote jambo ambalo linanifanya niwe kwenye ubora wangu muda wote.

Unaitazamaje Simba?

“Ni timu ya kipekee ndani ya Bongo imejipanga katika kila idara kuanzia uongozi na wachezaji wote wanatambua wanatakiwa kufanya nini na kwa wakati gani wafanye hayo mambo jambo ambalo linaifanya iwe hapa ilipo kwa sasa.

Ulikuwa Yanga na sasa Simba kwa nini?

“Maisha ya mchezaji na kazi anayofanya havimfanyi awe wa muda wote sehemu moja kwa wakati wote. Mchezaji anaweza kuhama timu moja kwenda timu nyingine kulingana na makubaliano na hicho ndicho kilichonitoa ndani ya Yanga na sasa nipo Simba naendelea kupambana.

Kuna kitu cha upekee ndani ya Simba?

“Ipo kuna upekee katika maisha hasa ukiangalia namna ambavyo ninaishi na wenzangu ndani ya Simba. Hapa sisi ni familia moja na kila mmoja anafanya jambo lake akitambua ni la familia.

Uzito wa mechi zenu za ligi upoje?

“Kila mechi ni ngumu na wachezaji wanatambua kazi ya kufanya  tunashirikiana katika kila mechi na kupeana majukumu ya kufanya hilo linatufanya tuwe tunapata matokeo kwenye mechi zetu tunazocheza.

Mechi yenu dhidi ya Yanga unaitazamaje?

“Ni mechi ngumu na kila mmoja anatambua kwamba kila tunapokutana na timu yoyote tunahitaji pointi tatu ambazo zitatufanya tufikie malengo yetu tuliyojiwekea.Tunawaheshimu wapinzani wetu na tunajua kwamba ni timu bora ila tutapambana ticheze tukiwa ni timu kwani tunazitaka pointi tatu zao ni muhimu kwetu kama ilivyo kwao.

Unadhani kuondoka kwako Yanga kumekuingiza kwenye uadui?

“Hapana, sina ugomvi na Yanga nina marafiki zangu pale nab ado tunawasiliana nao kwani mpira sio vita. Vita yetu sisi ni ndani ya uwanja baada ya hapo maisha yanaendelea ndivyo ilivyo duniani kote.

Unajutia kuondoka Yanga?

“Ni maamuzi yangu mwenyewe kuondoka sikulazimisha, hapa nilipo nina furaha nitazidi kupambana muda wote.

Vita yako na namba na Tshabalala ipoje?

“Naipenda na ni nzuri kwani hata nilipokuwa kulikuwa na ushindani wa namba. Kuhusu kuanza ama kutoanza hilo mimi silijui lipo mikononi mwa mwalimu.

Unafanyaje kuwa bora?

“Mazoezi na kujituma ndani ya uwanja pale ninapopata nafasi na kucheza kwa juhudi nikiwa mazoezini hata kwenye mechi pia,” anamalizia Gadiel.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic