January 3, 2020


WANASEMA kwenye soka vita ni vita na huwa haichagui silaha jambo la msingi ni kuona namna gani utajiokoa hapo ulipo na kubaki salama kwani kila mmoja atapambania timu yake ili ipate matokeo ikiwa ndani ya uwanja kwa muda wa dakika tisini.
Moto wa ndugu kwa mara ya kwanza utaonekana ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2019-20 ambapo Simba na Yanga zitamenyana kwa mara ya kwanza msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara.
Hesabu za kila shabiki, kila mchezaji ni kuona kwamba timu yake inaibuka kidedea kwa kusepa na pointi tatu jambo ambalo linaongeza utamu kwenye mechi hiyo ya watani wa jadi.
Ukiachana na tambo ambazo zinatawala kwa kila mmoja kama ilivyo ada kwamba siku zote mwamba ngoma huvutia kwake ndivyo ilivyo kwa hawa watani wa jadi ila ndani ya uwanja itakuwa ni vita kubwa ya ndugu wa kutoka taifa moja wakionyeshana umwamba wao.
Macho na masikio ya mashabiki ni kuona ni nani atakayemfunika mwenzake huku makocha wao wakimalizia mbinu zao kuona kwamba wanabeba pointi tatu bila kujali ugumu wa mchezo huo.

Pale ambapo mataifa kutoka nje ya nchi wanapokutana mahali pengine hawa huitwa ndugu kutokana na kuunganishwa na taifa lao, sasa hapa waliopo Bongo watauweka undungu pembeni kwa muda.
Kwenye timu hizi za Simba na Yanga kuna wachezaji ambao wanatoka taifa moja na watakuwa kazini Januari 4, kila mmoja akiwa upande wake akitetea ugali wake na nafasi yake upya kwenye timu yake ya taifa ni ndugu nje ya uwanja ila watakutana kwa mara ya kwanza kutafuta pointi tatu uwanja wa taifa:-
Shikalo vs kahata
Farouk Shikalo ni mlinda mlango wa Yanga yeye ni raia wa Kenya atakuwa na vita ya kibabe na kiungo mshambuliaji wa Simba Francis Kahata ambaye naye anatokea Kenya.
Shikalo ndani ya Kenya ana nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichoshiriki michuano ya Afcon nchini Misri ila hakuonyesha makeke yake zaidi ya kusugua benchi tofauti na Kahata ambaye yeye alipata nafasi ya kucheza kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika.
Watakutana Januari 4 kila mmoja akiwa na jukumu lake kubwa, Shikalo yeye anakazi ya kuzuia mashambulizi ya ndugu yake huyo mwenye asisiti nne na bao moja huku hesabu za Kahata ni kumtungua ndugu yake ama kutengeneza nafasi ya goli.
Yikpe vs wawa
Wote wanatokea nchini Ivory Coast, miili yao ni mikubwa na wanamitindo inayofana kwenye utembeaji isipokuwa mitindo ya nywele, Wawa ana kiduku ila Yikpe ni rasta.
Itakuwa ni vita ya ndugu hawa wawili uwanjani kwani Yikpe ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga yeye nafasi yake ni mshambuliaji na Pascal Wawa yeye ni beki.
Ndugu hawa kila mmoja ana malengo tofauti na mwenzake watapambana kuzipigania timu zao kwenye mechi iliyobeba hisia za mashabiki ambapo Yikpe atakuwa bize kutafuta ushindi huku Wawa akiwa bize kutibua mipango yake.
Molinga & Tshishimbi vs Kanda

David Molinga amekuwa gumzo kwa sasa ndani ya Yanga kutokana na uwezo wake licha ya kuwa na mwili mkubwa. anatokea Congo anacheza nafasi ya ushambuliaji ametupia jumla ya mabao manne atakuwa na vita na ndugu yake Deo Kanda ambaye ni kiungo mshambuliaji ndani ya Simba.
Kanda mwenye mabao mawili  asisti moja  mwenyewe hesabu zake ni kuvuruga mipango ya Molinga kati na kuwatengenezea wachezaji wake huku Molinga mwenye mabao manne akiwa na hesabu za kuwatungua Simba

Kagere vs Sibomana & Niyonzima
Kutoka Rwanda, Yanga itakuwa na nyota wawili ambao ni Haruna Niyonzima na Patrick Sibomana watamchangia Meddie Kagere kutoka Simba.
Niyonzima amerejea nyumbani baada ya msimu wa mwaka 2018-19 kutwaa ubingwa wa ligi akiwa na Simba ambayo alijiunga nayo akitokea Yanga shughuli yake uwanjani sio ndugu.
Sibomana ni nguzo kwa sasa kwa washambuliaji ndani ya Yanga amefunga jumla ya mabao manne na ametoa asisiti moja ya bao jambo linaloongeza vita yake na ndugu yake Kagere.
Kagere yeye ndiye kinara wa utupiaji ana mabao tisa ndani ya ligi na ametoa jumla ya asisiti mbili vita yao katikati inatarajiwa kuzimwa baada ya dakika 90.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic