January 19, 2020


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kilichowabeba mbele ya Yanga kwenye mchezo wao wa jana Uwanja wa Taifa ni morali ya wachezaji kucheza bila kuchoka.

Azam FC ilishinda kwa bao 1-0 mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Taifa mbele ya Yanga, bao pekee la Azam FC lilipatikana dakika ya 25 kupitia kwa beki kisiki, Ally Mtoni 'Sonso' ambaye alijifunga katika harakati za kuokoa kona ya Bruce Kangwa iliyopanguliwa na mlinda mlango, Farouk Shikalo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam, Jaffary Maganga amesema kuwa wachezaji walijituma bila kuchoka.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kuwa nafasi ya pili ikiwa imecheza jumla ya mechi 15 na ina pointi 32.

2 COMMENTS:

  1. MPIRA WA TANZANIA UNAHARIBIWA NA UPENZI WA KUPINDUKIA WA VIONGOZI WALIOPO NDANI YA VYOMBO VINAOUSIMAMIA MCHEZO WA SOKA KUIKANDAMIZA NA KUIONEA TIMU FULANI. RED CARDS BACK2BACK NA MAZINGIRA YANAFANANA. ATHARI ZAKE NI KWAMBA VIASHIRIA VYA VURUGU NA KUVUNJIKA KWA AMANI KATIKA VIWANJA VYA SOKA. PILI KUPUNGUA KWA HAMASA YA KWENDA VIWANJANI KWA MASHABIKI WA SOKA TATU, CHUKI YA MASHABIKI DHIDI YA VIONGOZI WANAOLISIMAMIA SOKA!

    ReplyDelete
  2. Acha kulazimisha usaha ugeuke kua damu kamwe haitakaa iwezekane,yanga ni jipu la usaha tena linahitaji kutumbuliwa haraka sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic