January 29, 2020


KOCHA wa Simba Sven Vandenbroeck amewasisitiza wachezaji wake kucheza kwa umoja ili kuendelea kupata ushindi utakaorudisha furaha kwa mashabiki na kutimiza malengo ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza Dar es Salaam amesema pamoja na kwamba wamekuwa wakiongoza ligi hiyo kwa utofauti pointi sita dhidi ya Azam na kushinda michezo yao iliyopita, lakini bado ajafurahishwa na ushindi huo pamoja na kiwango kinachooneshwa na wachezaji wake.

“Nahitaji wachezaji wangu wacheze kwa umoja ili kuendelea kupata ushindi utakao kuwa unarudisha furaha kwa mashabiki na kutimiza malengo yetu ya kutetea ubingwa wa ligi,” alisema Sven.

Amesema bado anatafuta mbinu ya kuinua ari ya wachezaji ili waweze kuendelea kufanya vizuri uwanjani ili kupeleka furaha kwa wapenzi na mashabiki
wa timu hiyo.

Sven amesema bado anatamani timu yake ifunge mabao mengi na kutoruhusu wapinzani wao kufunga bao lolote, ambapo anaamini kuwa kama kutakuwa na umoja, hilo linawezekana.

Kocha huyo ametolea mfano mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC walioshinda wa kitokea nyuma kwa mabao 2-1 wachezaji wake kunawakati walionekana wanategea kupokonya mipira hali iliyosabibisha lango lao wakati mwingi kuwa katika hatari.

“Changamoto hii nitaifanyia kazi kwenye mazoezi ikiwa ni maandalizi yetu kuelekea kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union ya Tanga kuhakikisha tunatumia kila nafasi kupata bao,” amesema Sven.

2 COMMENTS:

  1. Simba wawe makini kwenye benchi lao la ufundi kwani kuna viashiria tosha vya kuhujumiwa kwa kocha mpya.Moja ya sababu muhimu kabisa ya kuondolewa kwa Ausems ni fununu za kwamba alikuwa na urafiki uliopitiliza na wachezaji wake kiasi cha kupelekea nidhamu kupotea kwa baadhi ya wachezaji na kupelekea wachezaji kukosa kuwajibika ipasavyo uwanjani na hata kunako mazoezi. Amekuja kocha huyu mpya kiuhalisia mpaka hivi sasa timu anayofanya nayo kazi ni ya Ausems ila taratibu anaanza kuingiza mifumo yake ya kazi lakini tayari tunaanza kusikia vijinenoneno vinatokota chini kwa chini kutoka kwa baadhi ya viongozi na wachezaji yakwamba sijui Kocha mkali,sijui anaingilia majukumu yasio ya kwake,sijui anamwingilia kocha wa viungo,sijui ana maneno makali yaani ushuzi mtupu. Simba walitaka kocha alaiemakini na kazi yake asietaka mizaha ya kijinga. Kocha huyo wamempata na ni kocha anaeibadilisha timu uwanjani kutoka mbinu moja kwenda nyengine kulingana na ugumu wa timu husika uwanjani ili kuhakikisha timu inatoka na ushindi uwanjani kitu ambacho kilikuwa kikwazo kwa simba ya Aussems.Simba ilikuwa ikizibiwa mbinu zake za ushindi wakati wa Ausems basi walikuwa hawana mbinu mbadala ila sasa Tunaona utofauti upo. Tunasikia Meneja wa Simba anagombeana madaraka na kocha na kama hayo yanayosemwa ni kweli basi Simba wamuondoshe huyo meneja kwenye benchi la ufundi hata kama atakuwa anaheshima kiasi gani ndani ya Simba kwani ataikoroga timu.Simba sasa wanahitaji umoja ndani ya timu kwani ukiangalia mechi ya Simba na timu pinzani hata iwe dhaifu vipi lakini upinzani wanaokuja dhidi ya Simba ni waajabu. Ni dhahiri yakwamba timu hizi hupata nguvu za ziada kutoka kwa timu nyengine zinazotaka kuona Simba anadondosha points. Bila shaka kuna watu ndani ya benchi la ufundi la Simba walikuwa marafiki wakubwa wa kocha alieondoka ila wasitumike kutaka kumfelisha kocha huyu. Kocha apewe muda na ushirikiano wa kutosha na Majungu yakome kwenye benchi la ufundi au wenye Majungu wakomolewe. Mechi tatu zinazokuja za kufunga raundi ya kwanza ni zaidi ya fainali kuhakikisha timu inakaa pazuri na kukata kelele za vyura mitaani kwani kelele zimekuwa nyingi.

    ReplyDelete
  2. KOCHA ANAONEKANA ANAIJUA KAZI YAKE, HAPO KWENYE KUTEGEANA KUKABA NDIO SHIDA, LILE GOILI LA MWADUI NI KOSA LA KAHATA KWA KUSHINDDWA KUMALIZANA NA YULE ALIYE TOA PASI MAPEMA, HILI LILITOKEA KWA MUZAMIRU ILE MECHI YA YANGA NA KUPELEKEA MPAKA LEO MUZAMIRU KAPOTEA KABISA, NAFIKIRI ULINZI UNAANZIA MBELE, WASHAMBULIAJI NA MAWINGA WANATAKIWA WATAFUTE MPIRA PINDI WAKIPOTEZA SIO KUTEMBEA NA KUTEGEMEA MABEKI NA VIUNGO WAKABAJI WAFANYE HIO KAZI.. NI KWELI KUN WACHEZAJI SIMBA NI WAVIVU KUKABA LAKINI AWASISITIZE KUFANYA HIVYO.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic