January 29, 2020


Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison amesema anapofanya mbwembwe uwanjani halengi kuwadhihaki timu pinzani bali ni mahsusi kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki ambao wamelipa viingilio kuingia uwanjani

Aidha Bernard ameongeza kuwa hatafanya matukio hayo wakati wote, isipokuwa pale ambapo timu iko kwenye mazingira ya uhakika wa kuondoka na ushindi. Morrison ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kocha Luc Eymael kueleza kutofurahishwa na matukio hayo ambayo aliyafananisha na dhihaka kwa timu pinzani

"Mashabiki wanakuja uwanjani kuona timu yao inashinda, ndio maana wanalipa viingilio, lakini ninapoona timu inaongoza vizuri huwa naona ni bora kufanya kitu ambacho kitawapa burudani zaidi mashabiki wakienda nyumbani wapate cha kusimulia zaidi,"

"Nafikiri kocha yeyote hawezi kukubali hilo moja kwa moja, namheshimu kocha wangu (Eymael) kwa alichoniambia, lakini kwangu nafikiri kuna kitu cha ziada natakiwa kukifanya kama mchezaji, sidhani kama naweza kuacha lakini nitakuwa makini wakati gani nafanya hivyo"
Amesema Morrison.

Imeandaliwa na Yossima Sitta.

3 COMMENTS:

  1. Mcheza na majukwaa atapotea muda si mrefu.

    ReplyDelete
  2. Afuate ushauri wa mwalimu wake, mwalimu amezungumzia dhihaka lakini kuna suala la kujeruhiwa

    ReplyDelete
  3. Labda swala la kujeruhiwa nakubali lkn mengne tumeyashuhudia yakifanywa na Gaucho hata kipindi Manchester United anacheza na Barcelona nilshuhudia akifanya mbwembwe mbele ya beki kisiki Rio Fredinand.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic