January 3, 2020


TIMO Werner, mshambuliaji wa timu ya RB Leipzig na timu ya Taifa ya Ujerumani ameziingiza vitani Manchester United, Liverpool, Chelsea na Bayern Munich ambazo zinasaka saini yake.

Nyota huyo amekuwa na uwezo mkubwa ndani ya Uwanja jambo ambalo linawavutia mabosi wa timu nyingi na huenda kwenye dirisha hili lililofunguliwa mwezi Januari akasepa jumla na kwenda kati ya timu hizo.
Habari zinaeleza kuwa timu nyingi mbali na Chelsea ambazo zinashiriki Ligi Kuu England zinamuelewa kijana huyo mwenye umri wa miaka 23.
Anasifika kwa kucheza namba 10 ndani ya uwanja na amefunga jumla ya mabao 24 kwa ujumla ndani ya timu yake ya Taifa pamoja na klabu yake inayoongoza Bundesliga ikiwa na pointi 37.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic