January 3, 2020


USHINDI wa kwanza walioupata ndani ya mwaka 2020 umewafanya Azam FC waamini kwamba watafanya makubwa kwenye mashindano watakayoshiriki mwaka huu.

Azam FC, Januari Mosi, iliwafunga Singida United mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa ushindi huo unawapa furaha mashabiki na wachezaji kuendelea kupambana ndani ya mwaka 2020 kwenye mashindano yao yote.

"Tumeanza kwa hatua nzuri na kupata matokeo chanya, ushindani upo na tunajifunza kupitia makosa, kikubwa ni mashabiki kuendelea kutupa sapoti katika mechi zetu zote ili tufanye vizuri ni imani yetu itakuwa hivyo.

"Hii ni zawadi kwa mashabiki wetu na tuna amini mwaka huu 2020 utakuwa wa kipekee kwetu nasi tutaendelea kupambana," amesema.

Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza jumla ya mechi 13 ina pointi 26 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic