January 19, 2020



Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi timu ya Taifa ya Uganda kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Mechi ya leo ilikuwa ni ya kufuzu Kombe la Dunia litakalofanyika  Costa Rica na Panama, Julai 2-22  ambapo zilikwenda sare 
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kutafuta ushindi ambapo Uganda ilianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Nalukenge Juliet dakika ya 47 lililoongeza kasi kwa timu ya Tanzania na kuwafanya wasawazishe dakika ya 58 kupitia kwa Diana Lucas akimalizia pasi ya Asha Masaka.

Uzembe wa mabeki wa Uganda dakika ya 68 uliwapa zawadi ya kona Tanzania iliyopigwa na Diana Lucas na ikazamisha kimiani na Opah Clement.

Mechi ya marudio inatarajiwa kuchezwa Februari, Mosi nchini Uganda.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic