CRISTIANO Ronaldo, nyota wa Juventus amefikisha jumla ya mabao 50 akiwa kwenye maisha ya soka nchini Italia.
Nyota huyo mwenye miaka 35 alifikisha idadi hiyo wakati timu yake ikishinda mabao 3-0 mbele ya Fiorentina mechi iliyochezwa Jumapili.
Amefikisha mabao hayo 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 70 na kumfanya awe nafasi ya pili kwa watupiaji wenye mabao mengi 50 ndani ya muda mfupi.
Nafasi ya kwanza inashikiliwa na Icon wa AC Milan, Andriy Shevchenko aliyetupia mabao 50 baada ya kucheza mechi 69.
Mchezaji huyo alifunga mabao 29 msimu wake wa kwanza alifikisha jumla ya mabao 50, Januari, 21,2001 wakati timu yake iliposhinda jumla ya mabao 3-2 mbele ya Roma.
Nafasi ya tatu ipo mikononi mwa R9, Ronarldo, raia huyu wa Brazili ni majeruhi tu inaelezwa yalimchelewesha kufikisha mabao 50.
Alifikisha idadi hiyo akiwa na Inter kwenye mechi 77 mbele ya Piacenza, Oktoba 2,1999.
Marco Van Basten, Legend wa AC Milan anashika nafasi ya nne, alifikisha mabao 50 baada ya kucheza mechi 83 Januari 7,1990 mbele ya Cesana na alimaliza maisha yake ya soka akiwa amefunga jumla ya mabao 125.
Michel Platin yeye nafasi yake ni ya tano, alifikisha jumla ya mabao 50 baada ya kucheza mechi 84 akiwa na Juventus.
Ilikuwa Februari 26,1984 mbele ya Torino.

0 COMMENTS:
Post a Comment