February 9, 2020


RAHEEM Sterling nyota wa Manchester City leo atakosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya West Ham.

Nyota huyo ameumia nyama za paja na inasemekana kuwa huenda pia akakosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Pep Guardiola, Kocha Mkuu wa City amesema kuwa ni pigo kubwa na anafikiri ni miongoni mwa wachezaji waliowaweka kwenye wakati mgumu.


"Sterling ameumia na daktari ameshatuelekeza, nafikiri ngoja tuone lakini anaweza kurejea kabla ya mchezo dhidi ya Real Madrid," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic