February 23, 2020


PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa anatambua kwamba nyota wake Raheem Sterling anahitaji kuibukia ndani ya Real Madrid ambao wameonyesha nia ya kuitaka saini yake.
Imeelezwa kuwa Real Madrid na Barcelona ni miongoni mwa timu ambazo zimeonyesha nia ya kuipata saini ya nyota huyo na kutokana na timu hiyo kufungiwa kushiriki miaka miwili Ligi ya Mabingwa inatajwa kuwa shinikizo kwa nyota huyo kusepa.
Guardiola amesema kuwa anatambua nia ya timu hizo kubwa ambazo zinaitaka saini ya nyota yake na yote hayo yanatokana na uwezo mkubwa alionao.
Sterling hivi karibuni alisema kuwa naye anapenda kupata changamoto mpya na kubwa ila kwa kuwa sasa yupo Manchester City atapambana ndani ya klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic