February 26, 2020


UONGOZI wa Gwambiana FC inayoshirki Ligi Daraja la Kwanza umesema kuwa leo utaingia kwa hesabu kali mbele ya Yanga kwenye mchezo wao wa hatua ya 16 bora utakaopigwa Uwanja wa Uhuru.

Yanga itaikaribisha Gwambina saa 10:00 na mshindi wa leo atapenya hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.

Ofisa Habari wa Gwambina FC, Daniel Kirahi amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao ila hakuna namna nyingine watakayofanya zaidi ya kupata ushindi.

"Tunaingia kwa hesabu za kupata ushindi, wapinzani wetu tunawatambua wana uzoefu ila hakuna namna nyingine tutakayofanya tunahitaji ushindi.

"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao Uwanja wa Uhuru kwani kila kitu kinawezekana,".

2 COMMENTS:

  1. Gwambina piga mbwa hizo za porini watulie hao wanaitwa sare sare fc

    ReplyDelete
  2. gwambina yanga hawana ishu watoeni pumzi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic