February 26, 2020


SVEN Vandenbroeck Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kuna tatizo kubwa kwenye safu yake ya ulinzi jambo ambalo atalifanyia kazi kwa ukaribu.

Simba jana ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Stand United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na kushinda kwa penalti 3-2 kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho licha ya kuanza kufunga bao la kuongoza dakika ya 51 kupitia kwa Hassan Dilunga.

Sven amesema:" Wachezaji wanajituma ila nimegundua kuna tatizo kwenye safu ya ushambuliaji ni makosa ambayo tuliyafanya na tukaenda kuibukia kwenye penalti wakati mwingine tunak kazi ya kurekebisha makosa yetu,".

Bao la kusawazisha kwa upande wa Stand United lilifungwa dakika ya 67 na Miraj Saleh baada ya beki wa Simba kujichanganya.

2 COMMENTS:

  1. Jamani kweli Tuna tatizo .Kwenye maelezo mwandishi anadai kwamba Kocha Sven kasema timu yake ina tatizo Kwenye ulinzi kwenye direct quote Kocha anasema walipata tatizo Kwenye ushambuliaji ndio maana gemu ikafikia kwenye penalti!!!Which is which?Kwa sababu zote haziwezi kuwa kweli.Saleh Ally tusaidie.

    ReplyDelete
  2. ulinzi kwa simba bado ni tatizo hasa wakicheza hao akina hatuna na hao wenzake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic