Hivi ndivyo Saleh Jembe anavyoichambua Yanga na mikakati yake ya kutwaa ubingwa:-
Yanga bado haina mwendo mzuri maana iko katika nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 22.
Ina viporo viwili mkononi, ikishinda vyote itafikisha pointi 46 na kukwea hadi nafasi ya pili lakini itakuwa tofauti ya pointi 16 na vinara wa ligi hiyo Simba.
Kumbuka mechi zilizobaki kama idadi itakuwa ni 14 ili ligi kumalizika.
Pointi 14 ni sawa na kushinda mechi karibu tano. Maana yake, si kazi nyepesi kwa Yanga kuwa bingwa. Pamoja na hivyo inaonekana kuna kazi ya ziada kwa Yanga kwenda vizuri na lazima kurekebisha mambo kadhaa na namna moja katika ufungaji.
Yanga imefunga mabao 25 huku Simba ikiwa imefunga 50, mara mbili yake. Azam FC imefunga mabao 31.
ACHA UJINGA BROTHER,YANGA ANA KIBARUA KIKUBWA SANA MBELE YA SIMBA,AMEBAKISHA JUMLA YA MECHI 16 NA ANA ALAMA 41 INA MAANA UKIMPA ZOTE 48 ATAKUA NA ALAMA 89,SIMBA AMEBAKISHA MECHI 14 NA ANA ALAMA 62 UKIMPA MECHI 10 INA MAANA ATAKUA NA ALAMA 92,TAYARI HAPO PENYEWE KUNA TOFAUTI YA MECHI MOJA ILI YANGA AMFIKIE SIMBA AMBAPO INATENGENEZA JUMLA YA MECHI TANO ZA SIMBA KUPOTEZA ILI YANGA AWE BINGWA MSIMU HUU,HA HA HA HA POLE SANA MTANI.
ReplyDeleteKama unataka ubingwa msimu huu itabidi baada ya kuchukuliwa na mnyama wafanye mipango kuliiba kwa mitutu ya magongo laa si hivo wjaribu mwakani Mnyama huenda akawahurumia kutokana na mamilioni waliyoyahtumia Kununuwa Samaki waliochacha
ReplyDelete