Mkuu waWilaya ya Arumeru, Jerry Murro, leo amerejea klabuni Yanga na kuzungumza mambo kadhaa akiwapa wanachama matumaini kuwa yeye na wengine ambao hauwataja, wamerejea.
Baadhi ya kauli alizotoa, hizi hapa:
“Nimekuja nimeagizwa, kawaambie machozi yao sasa mwisho, hakuna mtu tena atalia ndani ya Yanga.
“Tunacheza na Gwambina, kesho ndio tunaanza, wachezaji watacheza ndani na sisi tutacheza nje. Tutaulinda uwanja na tutapambana na anayetaka kuionea Yanga.
“Tumezungumza na wachezaji, tutahakikisha wanapambana kufa na kupona, wachezaji wako tayari na sasa hatutaki ushindi wa bao moja bila.
“Potelea mbali, liwalo na liwe na tunataka kuanzia kesho watu wajue na wazikie kuna watu wamekerwa. Nawatangazia wananchi wenye timu yao, wale wengine ni mabwanyenye, msikate tamaa njooni uwanjani.
“Wachezaji wamelipwa, wananuka fedha na familia zao zijue na sasa wananuka fedha.
“Tumeimarisha ulinzi kambini, sasa tunapekua mitandao yao ya simu. Kama kuna wale wanaotuhujumu, tutawataja uwe Simba, uwe bodi ya uwe TFF.
“Ukichukua na wanachama wa Yanga undue umechukiwa na Mungu. Tunajua watu wamewekwa kutuhujumu mchana na usiku.
“Kama wewe wa mike, matopeni au mchangani utatukuta usiku, tunalinda timu yetu na nembo.
“Kumbukeni baada ya Magufuli ujue kinachofuata ni Yanga.
“Kumbukeni Yanga ilimpigania Haji wakati anaumwa macho. Mwacheni Nugaz aipiganie Yanga.
“Namuambia mmiliki wa Gwamibina awe makini, asikae karibu na Simba, atatupa hasira yutampiga nane.
“Sijarudi Yanga kama msemaji, nimekuja kama mwanachama na kiongozi mstaafu ninayeguswa. Password tulikuwa nayo sisi, nimerudi nayo pia.
Sasa ugonjwa wa macho yamekuja je?..hapo ndo Haji manara anapomind hata mie siwezi kukubali
ReplyDeleteKwani wewe uoni hata Hajj akiongea anatoa machozi!
DeleteEnter your comment...Ahsante muro kwa kututia moyo.
ReplyDeleteHapo ndipo tunapofeli kwenye mpira Imani za ushirikina, kuhongwa wachezaji siasa tunaacha kutafuta mapungufu ya timu zetu .. mpira ni taaluma tuwaache wataalam wafanye kazi zao siasa zina majukwaa yake
ReplyDeleteUsijifanye unashangaa ushirikina wakati timu yako na kagere wamekutwa na hirizi ndo zenu simba
DeleteHuyu ni kichaa
ReplyDeleteLalama fc hamuishiwi kulalama ila mungu atawalipa stahiki zenu,hamna timu alafu mnajifanya kudanganya uma kwa staili mnazojua wenyewe,poleni sana watani huyo muro ni mjasiriamali (inspiration man)anao uwezo wakuhamasisha ila wakati mwingine hutoka nje ya kitivo au kuruka mipaka ya kazi,hana muda mrefu huyo mtampiga chini wenyewe.
ReplyDeletehuwezi kujenga kwako kwa kutegemea kubomoa kwa jirani yako..ndiyo yale yale..kuna timu zinashinda kwa penalti...kama ni manji kumridisha aendelee ilishajaribiwa na hadi kupigiwa magoti!Yeye Jerry Muro ana shida gani endapo Simba viongozi wanaendelea? hivi yanga haikujua madhara ya kuleta wachezaji 20 wapya na benchi la ufundi jipya na uongozi mpya katika msimu mmoja...baada wa wimbo wa penalti, waamuzi kubeba, hujuma za tff na harufu vyumbani...sasa kisingizio ni kila mtu jangwani ni mpya wanazoeana...msisajili wapya tena ili wazoeane...Ya Simba mwachie Simba wewe chura fikiria namna gani utatoka matopeni ulimojidumbukiza mwenyewe
ReplyDeleteSemeni sana , ongeeni sana , sisi tunatii amri ya msemaji wetu kuwa tufunge midomo hadi baada ya tarehe 8 . Nami nafunga mdomo wangu
ReplyDeleteDomokaya lilimponza lomolomo, DC kichaa kuliko madc wote, he doesn't have qualities of leadership!!
ReplyDeletehirizi kwa simba ligi kuu tu
ReplyDelete