KOCHA Mkuu wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini amesema kuwa vijana wake wapo tayari kuzisaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa leo Uwanja wa Ushirika Moshi.
Hamsini amesema:-"Ni mchezo mgumu kwetu kwani wapinzani wetu wapo vizuri, nawatambua ila hilo halinipi shida, kikubwa ninachoamini ni kwamba vijana wangu wana juhudi na uwezo wa kupambana ndani ya Uwanja.
"Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Ushirika kuona namna mambo yatakavyokuwa, sapoti yao ni muhimu kwetu,".
Polisi Tanzania mchezo wake uliopita ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Yanga, inakutana na Ruvu Shooting liyotoka kuipapasa Coastal Union.







0 COMMENTS:
Post a Comment