February 22, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake hawajakata tamaa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu .

Yanga imeachwa kwa pointi 19 na vinara Simba wenye pointi 59 baada ya kucheza mechi 23 huku Yanga ikiwa nafasi ya nne na pointi 40 ikiwa imecheza mechi 21.

Eymael amesema:-"Wachezaji wangu nimekuwa nikizumgumza nao mara kwa mara na wanaonyesha kuwa na Imani ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu.


"Huwezi kukata tamaa ya kutwaa ubingwa ilihali bado kuna mechi nyingi za kucheza, nafasi hiyo ipo tutapambana kufikia malengo,".

Kesho, Yanga itakuwa kazini ikimenyana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

1 COMMENTS:

  1. HA HA HA HA HA NI KWELI KABISA LAKINI TAMBUA KWAMBA KUNYWA A.R.V AU KUPEWA USHAURI NASAHA HAKUTAKUFANYA UONDOKEWE NA VIRUSI VYA UKIMWI,HAYO NI KAMA MATUMAINI TU KWA MGONJWA JIPANGE KWA MSIMU UJAO,LQBDA UONGEZE MAJUNGU NA FIGISU ZAKUIDHOOFISHA SIMBA NA MASHABIKI WAKE KAMA MLIVYOKUA MNAFANYA JUZIJUZI,TUMEWASTUKIA HATA MFANYE NINI KAMWE HATUTETREKI TAFUTENI MBINU NYINGINE,THIS IS SIMBA NEXT LEVEL.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic