February 4, 2020

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa wachezaj wake wanacheza kwa juhudi wakiwa ndani ya Uwanja jambo ambalo linampa matokeo mazuri ndani ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa kila siku anaongea na wachezaji wake kuhusu mikakati mipya ndani ya timu jambo linalowapa nguvu ya kufanya kazi upya kwa upekee.

"Wachezaji wanatambua kwamba ligi ni ngumu na kila mmoja anatambua jukumu lake, kwa sasa ambacho tunakifanya ni kuongeza nguvu na morali kwa wachezaji kupata matokoe mazuri," amesema.

Mwezi Januari, Namungo FC imefunga jumla ya mabao 10 na imefungwa mabao nane kwenye mechi ilizocheza.

Mchezo wake wa kwanza mbele ya Simba msimu huu ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-2, Uwanja wa Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic