KIUNGO wa timu ya Liverpool, Adam Lalallana anajiandaa kwa sasa kusepa ndani ya kikosi hicho kilicho chini ya Jurgen Klopp.
Nyota huyo mwenye miaka 31, alimwaga wino ndani ya Liverpool, Julai, 2014, akitokea timu ya Southampoton.
Mkataba wake unameguka mwezi Juni hivyo atakuwa huru kujiunga na timu yoyote ile bure huku timu ya Arsenal ikipewa chapuo kuinasa saini yake.
Mchezaji huyo ameeleza kuwa mpango wake mkubwa ni kuona anacheza nje ya Anfield ili kupata changamoto mpya kwenye soka.
Mabosi wa Arsenal na Tottenham wote kwa nyakati tofauti wameonekena kuvutiwa na uwezo wa mchezaji huyo hivyo wanahaha kuipata saini yake.
Tottenham imempoteza mchezaji wao Christian Eriksen aliyetimika ndani ya Ligi Kuu England na kuibukia Serie A ndani ya Inter Milan mwezi Januari, Arsenal bosi Mikel Arteta yeye mpango wake ni kurejesha heshima ndani ya Emirates.
0 COMMENTS:
Post a Comment