February 8, 2020


MAMBO ni magumu ndani ya Simba kwa sasa baada ya kichapo cha bao 1-0 balaa zito limeibuka kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kwa kusema kuwa majeruhi wengi ndani ya kikosi wanawaumiza.

Sven Vandernbroeck amesema kuwa ameshindwa kupata matokeo mazuri kutokana na kuwa na majeruhi wengi ndani ya kikosi jambo ambalo hana ujanja nalo.

"kiukweli nina majeruhi wengi ndani ya timu yangu wapo sita wote ni wa kikosi cha kwanza, matokeo ya kufungwa ni mabaya siwezi kusema moja kwa moja kwamba wamechangia la ni suala linalohitaji muda," amesema.

Simba ipo nafasai ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 20 za ligi.

Jana, Februari, 7 ilifungwa bao 1-0 na JKT Tanzania mchezo wa Ligi Kuu Bara wa kwanza kwenye mzunguko wa pili.

4 COMMENTS:

  1. Wachezaji wazuri boko dilunga chama kahata huyo mbrazil ambae ni beki wote hao wapo nje na wapo kwenye benchi hawachezeshi maana yake nini afukuzwe hakuna kocha hapo kishingo huyo pesa nyingi tunatumia halafu upumbavu mtupu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mkuu kalime tikiti mpira huujui Simba nan mpka asifungwe au ni timu ipi duniani ambayo haijafugwa kwenye ligi zao nitajie 3 tu

      Delete
  2. Tatizo si kocha. Hatuna wachezaji wa kiwango. Yamebaki majina tu. Ukitaka kuamini ni siku hao wachezaji wavae jezi za Singida, watapigwa 5

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic