SINGIDA United iliyo chini ya Ramadhan Nswanzurimo imesema kuwa njia ya kuwabakiza kwenye ligi msimu ujao ipo mikononi mwa Mwadui hivyo lazima wapambane kupata pointi tatu.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 19 imeambulia ushindi mechi mbili, imepoteza mechi 13 na sare nne na pointi zake 10, nafasi ya 20.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana alimesema kuwa wachezaji wana morali kubwa ya kupata pointi tatu mbele ya Mwadui ili waitengeneze njia ya kubaki kwenye ligi.
“Tumekuwa tukishindwa kupata matokeo kutokana na kukosekana kwa muunganiko mzuri ndani ya timu ila kwa sasa tayari mambo yameanza kujipa, tutapambana kupata pointi tatu mbele ya Mwadui ambao watatufungulia njia ya kubaki ndani ya ligi.
“Timu nyingi zitashuka mwishoni mwa msimu hilo lipo wazi, tutakachokifanya ni kuongeza juhudi mara mbili zaidi ushindi utatupa hali ya kujiamini na kuongeza kasi ya kupambana kujinasua hapa tulipo,” amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment