February 15, 2020


TIMU ya Manchester City imefungiwa miaka miwili kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa UEFA na Shirikisho la Soka Barani Ulaya.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kukiuka sheria za matumizi ya fedha katika masuala ya usajili ndani ya mwaka 2012 na 2016.

Mbali na adhabu hiyo imepigwa faini ya pauni milioni 25 na maamuzi yanaruhusiwa kukatiwa rufaa na Manchester City.

Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa City, Pep Guardiola alipewa taarifa mapema ili awaandae wachezaji wake kisaikolojia kabla ya kupewa taarifa rasmi.

Taarifa rasmi kutoka UEFA imeeleza kuwa Manchester City haitakuwa na nafasi ya kushiriki michuano ya UEFA kwa muda wa misimu miwili kuanzia 2020/21 na 2021/22.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic