February 22, 2020


MBAO FC iliyo nafasi ya 16 na pointi zake 22 itakutana na Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mwadui FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 19 ilizojiwekea kibindoni baada ya kucheza mechi 22.

Wapinzani wa Mbao leo ni mafundi wa kulazimisha sare wakiwa nyuma ya Polisi Tanzania ambao ni vinara kwa kulazimisha sare ndani ya ligi.

Mbao imejipatia sare saba kwenye ligi na imefungwa mechi 10 miongoni mwa timu ambazo zimepanda daraja na zimesepa na pointi tatu ni Namungo FC iliyoichapa mabao 3-0.

Prisons imelazimisha sare 12 huku Mwadui FC ikiwa imelazimisha sare 10 kwenye mechi 22 ilizocheza.

Mwadui FC inahaha kutafuta ushindi wake wa nne ndani ya ligi na Mbao inatafuta ushindi wake wa sita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic