February 8, 2020


UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa haukufurahishwa na bao moja walilowafunga Yanga kwenye mechi yao ya kwanza, leo watafurahi wakiwafunga zaidi ya mabao matatu.
Ruvu Shooting, kwenye mchezo wa kwanza mbele ya Yanga Uwanja wa Uhuru ilifuta rekodi ya kufungwa kwenye mechi 18 walizokutana na Yanga sawa na dakika 1,620 kwa kupata bao moja lililofungwa na Sadat Mohamed.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema kuwa watafurahi wakiwafunga mabao zaidi ya matatu jambo litakalokuwa ni zawadi kwa mashabiki na viongozi wa timu.
“Tumekuwa tukishinda kwenye mechi zetu nyingi ila mabao ambayo tunayapata yamekuwa machache, mawili ama moja sasa wapinzani wetu Yanga tutafurahi tukiwafunga zaidi ya mabao mawili, iwe kuanzia mabao matatu italeta raha.
“Wao wanajidai kwamba wana watu ambao wanauchezea mpira hilo sisi halitusumbui kwani sisi tuna watu wanapiga mpira mwingi na pasi mpaka kwa golikipa mfano wa Barcelona,” alisema Bwire.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic